Madrid kipigo

 

Madrid kipigo cha pili La Liga





MADRID, HISPANIA.REAL Madrid imepokea kichapo cha pili kwenye Ligi Kuu ya Hispania, La Liga msimu huu, Villarreal ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Ceramica.

Villarreal inayonolewa na kocha wa zamani wa Barcelona, Quique Setien ilionyesha kiwango bora kwenye mchezo huo, dhidi ya mabingwa hao wa kihistoria wa Ligi Mabingwa Ulaya, huku kipa wa zamani aliyewahi kucheza Liverpool, Pepe Reina akikaa langoni.

Yeremy Pino aliwashangaza mashabiki wa Madrid baada ya kufunga bao la kuongoza dakika ya 47, kabla ya Madrid kusawazisha bao kwa mkwaju wa penalti dakika ya 60.


Hata hivyo Villarreal akapchika bao la pili kupitia Gerard Moreno aliyefunga kwa mkwaju wa penalti.

Licha ya Luka Modric na Vinicius Junior kutengeneza nafasi za kufunga, safu ya ulinzi ya Villarreal ilikuwa imara dakika zote za mchezo, Madrid ilikuwa na wakati mgumu na wakashindwa kufuruta mbele ya timu hiyo.

Baada ya kipigo hicho Madrid imeshuka nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kwa kutofauti ya mabao dhidi ya Barcelona licha ya kulingana kwa pointi 38.

Hadi tunaingia mtamboni Barcelina ilikuwa uwanjani ikicheza dhidi ya Atletico Madrid, endapo itapata ushindi watakuwa kleleni mwa msimamo kwa tofauti ya pointi tatu.

Comments