Mbappe amuumbua Rais

 

Mbappe amuumbua Rais wa Shirikisho Ufaransa





LONDON, ENGLAND. KYLIAN Mbappe amemtetea Zinedine Zidane kupitia ukurasa wake wa Instagram, baada ya Rais wa Shirikisho la Ufaransa kusema, hatapokea simu endapo mkongwe huyo atampigia kuulizia nafasi ya ukocha wa timu ya taifa.

Rais huyo Noel Le Graet amesema hatajali kwasababu hana imani na Zidane kama ataweza kubeba mikoba ya Denis Deschamps, lakini Mbappe amechukizwa na kauli hiyo.

Taarifa ziliripoti Zidane aligoma kuwa kocha wa Marekani, baada ya pendekezo kutolewa mkongwe huyo angekua chaguo sahihi la kubeba mikoba ya Didier Deschamps, kabla hajaongeza mkataba mpya hadi mwaka 2026.

Rais wa Shirikisho la Ufaransa (FFF) alizima uvumi huo baada ya tetesi kuibuka Deschamps alikuwa mbioni kuondoka baada ya fainali za Kombe la Dunia Qatar.

"Zidane alijaribu kuwasiliana na mimi? hapana, nisingepokea hata simu nyake, ningemwambia atafute klabu nyingine? aandae programu akatafute klabu au timu ya taifa atakayofundisha, sijali aende popote anapotaka, walidhani tungemuacha Deschamps? hapana, tunajua Zidane ana wafuasi wengi na jila lake siku zote anakuwa wa kwanza" alisema Rais huyo.

Lakni Mbappe akaibuka na kumjibu Rais hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter baada ya kauli yake hiyo ya kumdhalilisha Zidane aliyeipa mafanikio Ufaransa wakati analitumikia taifa hilo.

"Zidane ni Ufaransa, tusimkosee heshima nguli wa soka aliyefanya makubwa kwa taifa hili," aliandika Mbappe.
Nyota huyo anayekipiga Paris Saint-Germain alisifiwa kutokana kwa kauli yake na kumuunga mkono kwasababu Zidane alistahili kupewa heshima. 

Deschamps aliiongoza Ufaransa kutinga fainali ya Kombe la Dunia mara mbili mfululizo, mwaka 2018 aliipa ubingwa katika fainali zilizofanyika Urusi. Lakini katika fainali zilizofanyika Qatar, Ufaransa iliangukia pua dhidi ya Argentina.

Baada ya kupoteza ubingwa dhidi ya Argentina taarifa ziliripoti huenda Deschamps angeachia ngazi nafasi yake huku Zidane akipewa nafasi kubwa ya kuchukua mikoba yake.

Comments