Football

Mlandege bingwa Mapinduzi 2023, shoo ilikuwa ya kibabe





MABAO mawili ya Mlandege yaliyofungwa kipindi cha kwanza cha mchezo wametosha uipa ubingwa wa Mapinduzi 2023 na kuwafanya wanyakue Million 30 na medali za dhahabu huku Singida Big Stars ikilamba Million 20 na medali za fedha.

Baraza la wawakili Zanzibar imetoa Million 5 na kuifanya timu hiyo kuondoka na kitita cha Million 35 wakitwaa taji hilo baada ya miaka 13 mara ya mwisho timu za Zanzibar kutwaa taji ilikuwa ni 2009 wakichukua Miembeni.

Wakati wakitwaa taji hilo na kitita hicho timu hiyo imeahidiwa pikipiki aina ya Honda na mmiliki wake akitia kwa timu na benchi zima la ufundi Biemes Carno mchezaji bora mwenye nidhamu akipata laki tano huku mshambuliaji wa Mlandege Saite akilamba Million moja.

TIMU ZIMEGAWANA DAKIKA

Dakika 45 za kipindi cha kwanza Mlandege walicheza kwa kutulia na kutumia akili wakiwatuliza wapinzani wao SBS kila eneo wakifanikiwa kufunga mabao 2.

Mlandege walikuwa wanatumia mawinga wao kutengeneza mashambulizi walifanikiwa kwa kupata bao la kuongoza dakika ya saba kupitia kwa 18 kupitia Bashima Saul Saite.

Bao hilo liliamsha shangwe uwanja wa Amaan uliojaza mashabiki huku wachezaji wa Mlandege hawakuridhishwa na bao hilo moja waliendeleza mashambulizi kwa wapinzani dakika ya 18 mshambuliaji Abdulnassil Mohammed ambaye ni nahodha wa timu hiyo aliifungia timu yake bao la pili ambalo lilidumu hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Singida Big Stars walirudi kwa kutulia na kucheza mpira kwa kupasiana pasi za uhakika mshambuliaji wao Francy Kazadi pamoja na kupata ulinzi mkali alikwamisha mpira nyavuni dakika ya 51 likiwa ni bao lake la sita kwenye mashindano.

Bao la SBS liliwarudisha nyumba wachezaji wa Mlandege kwaajili ya kulinda mabao yao ya uongozi waliyoyapata kipindi cha kwanza huku wenyeji wa mchezo wakipambana kusaka bao la kusawazisha.

KAZADI CHINI YA ULINZI

Mfungaji bora wa mashindano ambaye ametupia mipira kambani mara sita kwenye mashindano ya Mapinduzi, Francy Kazadi ambaye alitupia mabao manne kwenye mchezo mmoja dhidi ya Azam FC na moja akiwafunga Yanga amewekwa chini ya ulinzi na mabeki wa Mlandege.

Singida Big Stars wamemuacha Kazadi kama mshambuliaji wa mwisho ameshindwa kuhimili mikikimikiki ya mabeki wa Mlandege ambao walionekana kuwa imara kulinda goli lao.

WAMEUJAZA

Licha ya Simba na Yanga ambao wamezoeleka kila wanapocheza uwanja wa Amaan wanaujaza, mchezo wa fainali kati ya Singida United dhidi ya Mlandege mashabiki wamejaza uwanja huo.

Mashabiki hao waliojitokeza kwa wingi kuipa sapoti Mlandege timu pekee ya Zanzibar iliyofanikiwa kuingia kwenye hatua hiyo baada ya miaka 10.

Mmiliki wa timu hiyo, Abdullsatal Said amenunua tiketi na kugawa bure kwa mashabiki wa timu hiyo ambao wameitikia wito na kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu hiyo.

TISHETI ZA UBINGWA MAPEMA

Timu ya Mlandege ni kama ilijua kuwa itatwaa taji hilo baada ya kutengeneza tisheti nyeupe na kuandika ‘Champions Mapinduzi 2023’ zikiwa na rangi nyeupe maandishi meusi na njano.

Comments